MWANAHABARI ALIYETEKWA ZANZIBAR AFUNGUKA RASMI,ATAJA KILICHOMPONZA,SOMA HAPO KUJUA
Salma Said, Mwandishi wa Habari wa Shirika la Utangazaji la Ujerumani (DW) na Gazeti la Mwananchi |
SALMA Said, Mwandishi wa Habari wa Shirika la
Utangazaji la Ujerumani (DW) pia Gazeti la Mwananchi amesema, licha ya kutekwa
na kuteswa hatorudi nyuma, anaandika Regina Mkondo.
Amesema, kazi yake ya uandishi
na kuripoti matukio mbalimbali ikiwa ni pamoja na yale yanayovunja haki za
binadamu itaendelea kama kawaida.
Amesema
hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ikiwa
ni siku mbili baada ya kutekwa na watu ambao hawakujitambulisha akiwa katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julisu Nyerere.
“Kupigwa
kwangu sio kitu kikubwa zaidi ya kuzuiwa kuandika na kuripoti habari, sababu
naamini wananchi walitarajia kusikia ripoti zangu na kufahamu hali halisi
inayoendelea visiwani Zanzibar,” amesema Salma.
Amesema,
wiki mbili kabla ya kufanyika uchaguzi wa marudio visiwani Zanzibar alipata
ujumbe wa vitisho uliomtaka kujihadhari juu ya kazi anazozifanya za kuripoti
taarifa ambazo ziliwakera baadhi ya viongozi.
“Kama
mnavyojua tangu kufutwa matokeo ya uchaguzi mkuu wa Zanzibar Oktoba 25, 2015
kulitokea mambo mabaya katikati ikiwemo ukiukwaji wa haki za binadamu kama
kupigwa, kutekwa na kutupwa nje ya mji,” amesema Salma na kuongeza;
“Sisi
tunaoijua Zanzibar tunayaona haya, kuna baadhi ya mambo hayaripotiwi na vyombo
vya habari kwasababu ya vyombo hivyo kupewa vitisho, lakini kwa waandishi
wanaoripoti katika vyombo vya nje kama Aljazeera walifanikiwa kuandaa
dokumentari ya matukio hayo.”
Salma
amesema, watekaji hao walimwambia kuwa ametekwa ili kuzuiwa kutoendelea
kuripoti habari za uchaguzi.
“Awali
nilipigiwa simu na kutumiwa ujumbe wa simu wa kunionya, nilikuwa nafuatwa hadi
ofisini kwangu, kuna siku nilifukuzwa na gari hadi nikadondoka chini,” amesema.
“Nimeteswa
kwasbabau ya kazi zangu za kutaka kutetea wananchi wenzangu na nchi yangu, kuna
siku nilihoji juu ya fedha kiasi cha biloni 7 zilizotumika kwa ajili ya
uchaguzi wa marudio, nahisi iliwakera baadhi ya watawala,” amesema.
Salma
amewataka waandishi wa habari kuacha kuandika habari za kufurahisha baadhi ya
watu huku wakiumiza wananchi bali waandike habari ambazo zinaeleza matatizo ya
jamii.
“Kama
mwandishi ni jukumu langu la kuhakikisha kuwa natoa msaada kwa jamii kupitia
taaluma yangu, nchi yetu ina matatizo mengi yanayohitaji kuripotiwa ili
viongozi wayajue na kuyatatua,” amesema.
Amewataka
waandishi wa habari kuwa na umoja na kuacha kuwakashfu baadhi ya waandishi
wanaopata shida kama alizopata yeye.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni